RONALDO AIPELEKA URENO NUSU FAINALI
BAO pekee la Cristiano Ronaldo dhidi ya jamhuri ya Czech usiku huu, limeiwezesha Ureno kutinga Nusu Fainali ya Euro 2012.
Ronaldo, ambaye alifunga mabao mawili dhidi ya Uholanzi, aling'ara sana kwenye mchezo wa leo kipindi cha kwanza hadi cha pili.
Lakini ilimbidi asubiri hadi zikiwa zimesalia dakika 12 mchezo
kumalizika ili kufunga bao hilo muhimu, akimtungua mmoja wa makipa bora
duniani kwa sasa, Petr Cech.
Ureno sasa itamenyana na mshindi kati ya Hispania au Ufaransa katika Nusu Fainali.
إرسال تعليق