SIMBA YASAJILI BONGE LA BEKI YONDAN CHA MTOTO

SIMBA YASAJILI BONGE LA BEKI YONDAN CHA MTOTO


Masomb

KLABU ya Simba SC, imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Masombo Lino kutoka Daring Club Motema Pembe.
Beki hilo la kati ambalo lilipiga soka ya uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lilitua jana Dar es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba.  
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema usiku huu kwamba beki huyo alikuwa ana mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa klabu yao, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ leo baada ya kutua jana na inawezekana leo amesaini mkataba wa miaka miwili.
“Masombo amekuja jana saa mbili usiku, alikuwa ana mzungumzo na Makamu Mwenyekiti, inawezekana leo akawa amesaini mkataba wa miaka miwili kama wameafikiana,”alisema Kamwaga usiku huu.  
Simba, mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, wanamsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari, Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani, Yanga.

1 تعليقات

  1. Simba haizibi pengo la Yondani bali inakiboresha kikosi kwa ajili ya michuano ya kimataifa

    ردحذف

إرسال تعليق

أحدث أقدم