UJERUMANI WAWAPUUZA CHELSEA WA MEDITERRANEAN

UJERUMANI WAWAPUUZA CHELSEA WA MEDITERRANEAN


Kikosi cha Ujerumani
Low, kocha wa Ujerumani
KOCHA wa Ujerumani, Joachim Low anaamini timu yake itashinda leo dhidi ya Ugiriki katika Robo Fainali ya Euro 2012 na amepuuza kauli kwamba wapinzani wao wanaiwakilisha 'Chelsea ya Mediterranean'.            Kauli hiyo imekuwa ikitolewa na vyombo vya habari vya Ujerumani na inatokana na jinsi Chelsea ilivyotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Bayern Munich.
Lakini Low amepuuza kufananishwa kwa kikosi cha Fernando Santos na klabu hiyo ya London Magharibi.
"Nimesikia habari mara chache kwamba wao ni Chelsea wa Mediterranean, lakini si kwa njia hiyo," alisema Low kuwaambia Waandishi wa Habari.
"Ugiriki wanacheza soka nzuri ya uelewano. Safu yao ya ulinzi ni imara, wako vizuri katika kupitia mipira miguuni mwa washambuliaji na kuzuia na kushambulia kwa kushitukiza ipo kwenye damu yao.
"Wamekuwa wakicheza hivyo kwa miaka mingi. Ni kama ilivyokuwa mwaka 2004 [wakati walipoibuka mabingwa wa Ulaya nchini Ureno]."Walipotea wakati fulani, lakini wakati wote wapo juu. Lakini kwa vyovyote, Chelsea wanacheza tofauti [mtindo wa] soka tuliouona kwenye fainali au Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa."
Timu hizo zimefuzu kutinga Robo Fainali kwa mazingira tofauti. Die Mannschaft walifuzu kutoka kundi lao kwa kubeba pointi zote, wakati Ugiriki walifuzu kwa kujikusanyia pointi nne, wakishinda mechi ya mwisho dhidi ya Urusi na kujihakikishia kusonga mbele.
Low anafahamu kwamba timu yake inatarajiwa kusonga mbele Nusu Fainali, na licha ya kutishwa kwamba wapinzani wao ni hatari, lakini bado ana matumaini na timu yake itasonga mbele.
"Kwa kutumia akili, tunapewa nafasi, lakini tutalifanyia kazi hilo. Lakini kumbuka mechi za mtoano zina desturi yake, hivyo haitakuwa kwamba anayepewa nafasi lazima asonge mbele.
"Tumeona katika hatua ya makundi wakati Urusi, ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kusongta mbele na wote tumeona nini kilitokea.
"Lakini kama tutaonyesha uwezo na nguvu zetu zote, kisha tuna imara kiasi cha kutosha kuwafunga Ugiriki. Nashawishika tutashinda."alisema. Mechi hiyo itaanza saa 3:45 usiku.

Post a Comment

أحدث أقدم