USAJILI BARA KUFUNGWA AGOSTI 10, SIMBA AZAM KUCHEZA NGAO AGOSTI 25
Danny Mrwanda amesaini Simba SC |
KIPINDI
cha kwanza cha usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu wa 2012/2013
kitamalizika Agosti 10 mwaka huu kulingana na kalenda ya Matukio ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya 2012/2013.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo ameongea jioni
hii kwamba, uhamisho wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Julai
30 mwaka huu wakati kipindi cha kuacha wachezaji (sio wa Ligi Kuu.
Wachezaji wa Ligi Kuu wanacheza kwa mikataba) ni kuanzia Juni 15- 30
mwaka huu.
Amezitaka klabu
za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni
kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia
Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.
Frank Damayo amesaini Yanga SC |
“Tunasisitiza
kipindi cha usajili kiheshimiwe na mikoa yote kwa sababu usajili huo huo
ndiyo utakaotumika katika michuano ya Kombe la FA. Kwa maana nyingine
hakutakuwa na kipindi kingine cha usajili wa wachezaji kwa klabu zote
nchini hadi hapo litakapofunguliwa dirisha dogo,”amesema.
Mechi ya
kufungua msimu ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kati ya mabingwa wa
Ligi Kuu, timu ya Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Agosti 25 mwaka
huu wakati Ligi Kuu itaanza Septemba Mosi mwaka huu, na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) yenyewe itaanza Septemba 15 mwaka huu.
Ratiba ya Ligi Kuu itatolewa Julai 23 mwaka huu.
Post a Comment