Walimu wasisitiza mgogoro upo palepale

http://www.eatv.tv/media/picture/large/pix%202(1).jpgWAKATI mgomo wa madaktari umesitishwa na Serikali, Chama cha Walimu  Tanzania (CWT), kimesema maandalizi ya mgomo wao yanaendelea iwapo Serikali haitatekeleza makubaliano yao watafanya mgomo usio na mwisho kuanzia Julai 16, mwaka huu.
Mgomo huo utaanza kama Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA) haitatoa uamuzi wa kuridhisha  utakaotolewa Juni 26, mwaka huu.
CWT kilisema iwapo hakitaridhishwa na uamuzi huo, walimu nchi nzima watapiga kura za siri kuhusiana na matokeo hayo, kisha kutoa notisi ya saa 48 kabla ya kuanza mgomo.
Pia, kilisema hakijatangaza mgomo bali kilichopo ni mgogoro ambao kama Serikali itashindwa kutekeza mapendekezo na makubaliano waliyotoa, wanaweza kupelekea kufikia mgomo nchi nzima.
Akizungumza kwenye mjadala wa kiashirio cha ajira ulioshirikisha viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi  Tanzania (Tucta) na Chama cha Waajiri Tanzania (Ate), Mkuu wa Idara ya Utetezi Walimu na Mwanasheria wa CWT, Leonard Haule, alisema hivi sasa imetangaza mgogoro na Serikali.
Haule alisema mgogoro huo unatoa fursa ya majadiliano au utekelezaji madai yao, iwapo mwafaka hautafikiwa Julai 16, wataanza rasmi mgomo nchini nzima.
“Sisi hatujatangaza mgomo wa walimu, bali tumetangaza mgogoro ambao kama mambo tuliyoyataka hayatatekelezwa, basi unaweza kupelekea  mgomo,” alisema Haule.
Alisema Juni 5, mwaka huu mkoani Dodoma, CWT ilipitisha azimio la kutangaza mgogoro kwa lengo la kutaka Serikali kutekeleza yale waliyokubaliana kuhusu nyongeza za mishahara, posho za kufundishia na posho kwa walimu wanaofundisha katika mazingira magumu.
Alitaja madai yao kuwa, ni nyongeza ya mshahara kwa asilimia 100, posho ya ufundishaji ambayo kwa walimu wa sayansi wanataka walipwe asilimia 55 ya mshahara wao kila mwisho wa mwezi na asilimia 50 kwa walimu wa masomo mengine.
Mengine ni posho ya mazingira magumu yanayotambuliwa na Serikali kwa walimu, ambayo ni asilimia 30 ya mshahara kwa kila mwalimu
 

Post a Comment

أحدث أقدم