Polisi
na mamlaka ya wanyama pori nchini Kenya wapo katika msako mkali
kuwatafuta wakazi wa Kitengela walioua simba sita kutoka hifadhi ya
taifa ya Nairobi.
Simba hao wanaodaiwa kuvamia na kuua kondoo 28 siku ya jumatono asubuhi.
Mkurugenzi
wa huduma za wanyama pori Julius kipng’etih amedhibitisha mauaji hayo
ya simba 6 na kondoo 28, na kusema Simba hao walipotea kutokea hifadhi
ya Nairobi.
“nilazima tuwakamate waliohusika na mauaji haya ya Simba, wanapaswa kupambana na sheria” alisema mkurugenzi huyo.
Simba
hao waliua ng’ombe 8 siku ya jumatatu, na hivyo wakazi wa eneo hilo
kukosa uvumilivu baada ya Simba kuua tena kondoo siku ya jumatano.
إرسال تعليق