JINAMIZI linazidi kuwaandama wasanii wa tasnia ya filamu baada ya mwanadada mwenye mikasa kutoka Bongo movie Wema Sepetu kumwaga chozi back stage wakati mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo fleva Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ alipopanda Jukwaani na kusema Bongo fleva ni kicheche kama Wema Sepetu.
Chanzo chetu cha habari kimesema
kuwa Ney alipopanda Jukwaani na kuchana freestyre na kulinganisha
Bongofleva kicheche kama Wema Sepetu umati uliokuwa uwanjani ulilipuka
kwa furaha na kumshangilia Ney akiwa sambamba na Dallaz Ukuni
mwanamuziki mwenzake.
Kufuatia hali hiyo Jacob Stephen ‘JB’, Aunt Ezekiel wakiwa na Steven Nyerere walizua zogo lilotengeneza fujo wakitaka kumvamia Ney na kumpiga huku JB akilalama kwa kusema kuwa Ney amekuwa akiwadhalilisha kwa kutumia nyimbo zake.
Wakati hayo yakifanyika Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ alionyesha busara zake kwa kutoshiriki ugomvi huo.
.

Aunty Ezekiel na Wema wakiwa wamejiachia
“Sasa hawa
mbona wanataka kutuharibia show yetu vipi? Kwanza huyu aliyeitwa
kicheche hata hajamaindi lakini wapambe ndio nawaona wanataka
kulianzisha mbona mwenzao Ray katulia?" alihoji Samson Masanja mkazi wa Mwanza.
Pamoja na sakata hilo show ilibamba kwa msanii Ney wa Mitego Dallaz Ukuni kufanya bonge la show sambamba na wasanii wengine wakali wa Bongo fleva kama Roma, Fid Q, Bob Junior, Mwasiti, Godzilla, Barnaba, Pro. Jay, Recho, At na Nyota kutoka THT

Post a Comment