MAGAZETI LEO HII ULAYA:- UPANDE WA SOKA

ROONEY ATOA KITABU KIPYA, AMZUNGUMZIA FERGUSON

Alessandro Del PieroKatika kitabu chake kipya, mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kutemwa na kocha Sir Alex Ferguson lilikuwa somo kubwa kwake. (Daily Mirror)
Mshambuliaji Sergio Aguero 'amemtibua' kocha wake Roberto Mancini kwa kuamua mwenyewe kwenda kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na Argentina, wakati kwa sasa hayuko fiti hata kuitumikia klabu yake, Manchester City.
Mshambuliaji Lukas Podolski, mwenye umri wa miaka 27, anaamini Arsenal wanaweza kuwa washindaji wa taji kama wataendelea na staili yao ya Jumapili, walipoifunga Liverpool.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood amesema The Gunners hawawezi kushindana na Chelsea na Manchester City katika soko la usajili.
Mashabiki wa Liverpool wa kikundi cha Spirit of Shankly, wamemtaka, Mmiliki MMarekani wa klabu hiyo, Fenway Sports Group kuteua Mtendaji Mkuu mkazi wa Liverpool.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alitaka kubadilishana wachezaji, kiungo Jordan Henderson, winga Stewart Downing au beki wa kushoto, Jose Enrique ili kumpata mshambuliaji wa Fulham, Clint Dempsey, ambaye alitaka kwenda Tottenham.

Post a Comment

Previous Post Next Post