ROONEY ATOA KITABU KIPYA, AMZUNGUMZIA FERGUSON
Mshambuliaji Sergio Aguero 'amemtibua' kocha wake Roberto Mancini kwa
kuamua mwenyewe kwenda kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na
Argentina, wakati kwa sasa hayuko fiti hata kuitumikia klabu yake,
Manchester City.
Mshambuliaji Lukas Podolski, mwenye umri wa miaka 27, anaamini
Arsenal wanaweza kuwa washindaji wa taji kama wataendelea na staili yao
ya Jumapili, walipoifunga Liverpool.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood amesema The
Gunners hawawezi kushindana na Chelsea na Manchester City katika soko la
usajili.
Mashabiki wa Liverpool wa kikundi cha Spirit of Shankly,
wamemtaka, Mmiliki MMarekani wa klabu hiyo, Fenway Sports Group kuteua
Mtendaji Mkuu mkazi wa Liverpool.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alitaka kubadilishana
wachezaji, kiungo Jordan Henderson, winga Stewart Downing au beki wa
kushoto, Jose Enrique ili kumpata mshambuliaji wa Fulham, Clint Dempsey,
ambaye alitaka kwenda Tottenham.
إرسال تعليق