Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akionyeshwa ramani ya
eneo la chuo cha sayansi ya Afya Mbweni na msimamizi wa ujenzi wa chuo
hicho Bw. Waziri Juma ambalo limeshapimwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi.
Jengo
la Bw. Abdulla Ali Khamis ambalo limo ndani ya eneo la chuo cha Sayansi
ya Afya Kilichopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa
Polisi wa Nchi wanachama wa Mataifa ya Kusini, Mashariki na Kati mwa
Afrika SADC nje ya Ofisi yake baada ya kufanya nao mazungumzo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza mwanachama
mpya aliyejiunga katika Jumuiya ya wachangiaji damu kwa Hiari Zanzibar
Bibi Maryam Mohd akichangia damu kwa mara ya kwanza katika kituo cha
damu salama Kiliopo Sebleni Mjini Zanzibar.
Jengo
jipya la Bohari Kuu ya Wizara ya Afya linaloendelea kujengwa ndani ya
eneo la kiliokuwa kiwanda cha Sigara Maruhubi Mtoni.(Picha na Saleh
Masoud Mahmoud – OMPR- ZNZ).
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anakusudia kumuandikia
Barua Waziri anayesimamia masuala ya Ardhi Zanzibar kumtaka kufuta mara
moja hati ya umiliki wa Viwanja vya nyumba ambavyo vimo ndani ya eneo
la Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni.
Balozi
Seif ametoa kauli hiyo wakati akiangalia eneo la Chuo hicho ambalo
limevamiwa kwa ujenzi, wakati wa ziara yake katika Taasisi zilizomo
ndani ya Sekta ya Afya ikiwa ni mwanzo wa ziara zake kuangalia utendaji
wa Wizara za Serikali pamoja na changamoto zinazozikabili Wizara hizo.
Balozi
Seif akionyeshwa kukasirishwa kwake na tabia ya baadhi ya watu kukaidi
maamuzi ya Serikali pamoja na Maagizo ya Mahakama ya kuhodhi ardhi
amesema Taifa halitakuwa na Maendeleo kama Jamii ikijali zaidi Ubinafsi.
Ameagiza
kusitishwa mara moja maendeleo ya ujenzi wa nyumba moja ambayo tayari
ina mgogoro ulioko mahakamani pamoja na kuzuiwa kwa ujenzi wowote kwa
wale waliomilikishwa viwanja saba ndani ya eneo hilo la chuo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefahamisha kwamba Serikali haikusudii
kufanya ubabe kwa raia wake lakini kamwe haitasita kumchukulia hatua za
kisheria Raia atakayeonyesha dharau au jeuri dhidi ya Serikali.
Ameoupongeza
Uongozi wa Wizara ya Afya kupitia Chuo hicho kwa juhudi zake za
kuendeleza Majengo yatakayokidhi mahitaji ya wanafunzi kwa siku za
baadae.
Mapema
Msimamizi wa Ujenzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni Ndugu Waziri
Juma alimueleza Balozi Seif kwamba Eneo hilo lilikuwa likimilikiwa
kihalali na Chuo cha Ufundi cha Mbweni tokea mwaka 1962.
Ndugu
Waziri alisema Chuo cha Sayansi kililazimika kisheria kuomba eneo hilo
kwa ajili ya ujenzi wa chuo chake ambapo baadaye uongozi wa chuo hicho
ukaamua kujenga ukuta baada ya kuanza dalili za uvamizi wa eneo hilo.
إرسال تعليق