KIKOSI
cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba kimezidi
kuimarika baada ya mshambuliaji wake wa Kimataifa, Emmanuel Okwi kurejea
jioni ya leo na anatarajiwa kuungana na wenzake katika mazoezi
yanayoendelea kwenye
viwanja vya TCC Chang’ombe.
Okwi alikuwa akiitumikia timu yake ya Taifa ‘The Cranes’ ambayo
jana ilicheza mechi ya kuwania nafasi 15
za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani na kufungwa bao 1-0 anatarajiwa kuwa
miongoni mwa wachezaji wa Simba watakoshuka katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam
keshokutwa kukipiga na Azam Fc katika mchezo maalum wa kuwania Ngao ya jamii
(Community Shield).
Ofisa habari wa
Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba ujio wa Okwi makali ya timu hiyo katika
mchezo wao na Azam kesho pamoja na ligi kuu kwa ujumla inayotarajiwa kuanza
kutimua vumbi Septemba 15.
Alisema kikosi cha Simba kipo katika hali nzuri kikiendelea
na maandalizi yake ya mchezo huo huku
pia mshambuaji wake mwingine wa kimataifa Mzambia Felix Sunzu
aliyekwenda kumzika dada yake Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) akitarajiwa
kuwasili leo.
إرسال تعليق