MOJAWAPO KWA
Cristiano Ronaldo (pichani akiwasili mazoezini jana) |
KLABU
zenye 'hela chafu', PSG, Manchester City na Chelsea zinajipanga kumtwaa
Cristiano Ronaldo, baada ya mshambuliaji huyo kusema hana furaha Real
Madrid.
Ronaldo aligoma kushangilia mabao yake Real Madrid Jumapili na akasema baada ya mechi hiyo ni sababu za kimchezo.
Ronaldo anaingia Bernabeu |
Klabu
hizo tajiri kiasi cha kutosha zinaweza kutoa pauni Milioni 100 kuvunja
mkataba wake Real uliobakiza miaka mitatu na zinaweza kumpa mshahara
kuanzia pauni Milioni 1 kwa mwezi.
Jose
Mourinho pia hatarajiwi kubaki Real, kuna uwezekano akaondoka msimu
ujao na anaweza akamtanguliza Ronaldo sehemu atakayokwenda, zaidi City
na PSG zikipewa nafasi kubwa.
Mshambuliaji
huyo Mreno, alisajiliwa kutoka Manchester United kwa pauni Milioni 80
mwaka 2009, na hadi sasa ameipa Real taji la La Liga msimu uliopita,
akifunga mabao 46 katika mechi 38 na mabao 60 katika mashindano yote,
kiwango ambacho mchezaji huyo mwenhye umri wa miaka 27 anafikiri
hakiendani na maslahi duni anayopata hapo.
Amefunga
mabao 150 katika klabu hiyo, kiwango ambacho ni zaidi ya bao moja
katika kila mechi, lakini bado anafunikwa Lionel Messi wa Barcelona.
Wengine wanasema Messi ndiye anayemnyima raha kiasi cha kufikiria
kuondoka.
Ronaldo alitolewa Jumapili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Granada Uwanja wa Bernabeu baada ya kuumia
Aliwapungia tu mikono mashabiki baada ya kufunga juzi
Wakati
alipoboronga akiichezea timu yake ya taifa, Ureno dhidi ya Denmark
katika Euro 2012, mashabiki wa Denmark walimzomea wakitaja jina la
Messi.
Ronaldo
hapewi hadhi kubwa Real kama Messi anayopewa Barca na kituo kimoja cha
Redio kiliripoti kwamba alikuwa na mazungumzo na raia wa klabu,
Florentino Perez akilalamikia kutopewa sapoti katika chumba cha
kubadilishia nguo.
Lakini pia na kukosa tuzo ya Mwanasoka Bora Ulaya mbele ya Andres Iniesta wiki iliyopita, kunaongeza machungu kwenye moyo wake.
Ronaldo akiwa benchi baada ya kutoka Jumapili
Post a Comment