Mwandishi wa habari za michezo
Shaffih Dauda ameripoti kwamba Siku moja baada ya kamati ya sheria,
maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF kutoa maamuzi juu ya mapingamzi ya
Simba dhidi ya wachezaji Kelvin Yondani na Mbuyu Twitte kuichezea klabu
Yanga – kwa kuwaidhinisha wachezaji hao kuichezea Yanga. Leo hii klabu
ya Simba imesema inafikiria hatua za kuchukua juu ya uamuzi huo wa
kamati ya Alex Mgongolwa.
Kwa taarifa za kuaminika
alizozipata Shaffih kutoka ndani ya uongozi wa Simba ni kwamba kamati ya
utendaji ya klabu hiyo itakutana usiku wa leo kujadili hatua za
kuchukua huku baadhi ya wajumbe wakisema kutokana na uonevu wanaotendewa
na TFF itabidi wajitoe kushiriki kwenye ligi kuu kwa sababu hawana
imani na shirikisho hilo.
Simba inalalamika kwamba
wachezaji wote wawili Mbuyu Twitte na Kelvin Yondan wamesajiliwa na
Yanga isivyo halali. Kwa upande wa Twitte walitaka walipwe fedha zao
$32,000 walizompa mchezaji huyo na akasaini nao mkataba kabla ya Yanga
kuwazidi kete na kumsainisha mkataba mpya beki huyo aliyekuwa akiichezea
APR ya Rwanda, na pia walitaka Twitte afungiwe kwa sababu alisaini
mkataba na kalbu zote mbili kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kwa upande wa Yondani Simba
wanadai mchezaji huyo ni halali yao kwa sababu bado ana mkataba na klabu
hiyo, pia wakataka Yanga iadhibiwe kwa kitendo cha kufanya mazungumzo
na mchezaji ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya zamani lakini
jana kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF ikatoa
maamuzi ya kuwaidhinisha Twite na Kelvin Yondan kwenda Yanga, maamuzi
ambayo Simba wamesema sio sahihi.
Source: www.shaffihdauda.com
إرسال تعليق