KOCHA Mkuu wa
Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet ameteua wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya
ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya Prisons Jumamosi kwenye
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, Saintfiet alisema ameteua
wachezaji hao kulingana na mazingira ya mechi yenyewe na kwamba wachezaji
wengine wote waliobaki ni wazuri pia.
Aliwataja wachezaji
aliowateua ambao wanaondoka kesho asubuhi kuwa ni makipa; Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Shadrack Nsajigwa,
Juma abdul, Godfrey Taita, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, David Luhende, Oscar
Joshua na Stefano Mwasyika.
Aliwataja
viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Nizar
khalfan, Shamte Ally na Simon Msuva, wakati washambuliaji ni Jerry Tegete,
Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza.
Aliwataja wachezaji
wa kikosi cha kwanza ambao hawatasafiri kwa ajili ya mechi hiyo kuwa ni kipa
Said Mohamed, Ladislaus Mbogo, Job Ibrahim, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Omega
Seme, Nurdin Bakari, Idrisa Assega na Issa Ngao wa Yanga B, ambaye anakomazwa
kikosi cha kwanza.
إرسال تعليق