Al-Shabaab yazidisha hali ngumu ya kibinaadamu kwa kuyafukuza mashirika ya msaada

Mwanamke wa Kisomali akimbeba binti yake wa miezi 7 katika hospitali moja mjini Mogadishu baada ya kugeuzwa kuwa mkimbizi wa ndani kutokana na ukame na maradhi. Mashirika mengi ya msaada hayawezi kuwafikia Wasomali wenye uhitaji mkubwa katika maeneo yaliyo chini ya al-Shabaab, kuzidisha mgogoro huo. [Roberto Schmidt/AFP]
Na Majid Ahmed, Mogadishu

Amri ya al-Shabaab kuyapiga marufuku mashirika ya msaada ya kiutu katika maeneo inayoyadhibiti kunazidisha mgogoro wa kibinaadamu nchini Somalia na kuhatarisha maisha ya maelfu ya wahanga wa njaa, wasema maafisa wa serikali na wafanyakazi wa msaada.



Tarehe 8 Oktoba, al-Shabaab ililipiga marufuku shirika la msaada la Islamic Relief la Uingereza kufanya kazi zake katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake, ikililaumu shirika hilo kwa kufanya kazi kwa siri na mashirika ya msaada ambayo kundi hilo ilishayafukuza. Shirika la Islamic Relief limekuwa likifanya kazi nchini Somalia tangu mwaka 2006.

"Islamic Relief imeshindwa mara kadhaa, licha ya onyo la mara kwa mara, kuheshimu miongozo ya kufanya kazi iliyowekwa na OSAFA (Ofisi ya al-Shabaab ya Kusimamia Masuala ya Mashirika ya Msaada)," al-Shabaab ilituma taarifa yake kwenye Twitter. "Islamic Relief pia iligundulika kutanua huduma zake kwa siri kwa mashirika yaliyopigwa marufuku, hasa WFP (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani), katika maeneo yaliyo chini ya HSM [Harakat al-Shabaab al-Mujahideen]."

Islamic Relief ilikana tuhuma hizo. "Hakuna hata programu yetu moja nchini Somalia inayofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani," alisema Iftikhar Shaheen, mkurugenzi wa shirika hilo kwa kanda ya Afrika ya Mashariki, katika taarifa yake. "Ikiwa uamuzi huu utathibitishwa, utayatia hatarini maisha ya watu wengi, kuhatarisha kazi yetu ya kutoa chakula, maji, huduma za usafi na tiba na msaada kwa ajili ya kuongeza kipato kwa watu milioni 1.3 nchini Somalia."

Amri hiyo ya kupiga marufuku shirika la Islamic Relief ni ya karibuni kabisa katika mtiririko wa amri kama hizo dhidi ya mashirika ya msaada ya kimataifa. Katika mwezi Machi, al-Shabaab ililipiga marufuku shirika la kuhudumia watoto la Save the Children, na katika mwezi wa Januari, kundi hilo lilitoa amri kwa shirika la Msalaba Mwekundu kuacha kufanya operesheni zake. Katika mwezi Novemba 2011, kundi hilo liliyapiga mashirika 16 ya kimataifa kufanya kazi katika maeneo linayoyadhibiti, likiwemo Shirika la Afya Duniani na mashirika makubwa ya Umoja wa Mataifa.

Mnamo mwaka 2010, al-Shabaab pia ililipiga marufuku shirika la Mpango wa Chakula Duniani, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Idara ya Umoja wa Mataifa ya Usalama, shirika la kimataifa la Mercy, shirika la kimataifa la Oxfam, Shirika la Maendeleo la Italia, shirika la Msaada la Kiislamu na shirika la Kimataifa la Care.

Serikali ya Somalia imelaani hatua hiyo ya al-Shabaab. "Uamuzi wa al-Shabaab kuyafukuza mashirika ya kibinaadamu kutoka maeneo inayoyadhibiti unayatia hatarini mamia kwa maelfu ya maisha ya watu, hasa wanawake na watoto," alisema Abdullahi Jimale, mkuu wa Shirika la Taifa la Kupambana na Majanga.

"Amri hii ya al-Shabaab ya kupiga marufuku mashirika ya msaada yanaifanya hali ya kibinaadamu kuwa mbaya zaidi na kuyafanya maisha ya watu kuzidi kuwa magumu," aliiambia Sabahi. "Tunawatolea wito al-Shabaab kujiepusha na kuweka siasa kwenye masuala ya msaada ya kibinaadamu, inayokusudiwa kuyanusuru maelfu ya maisha ya watu wenye uhitaji mkubwa."

Jimale aliitaka al-Shabaab kuyaruhusu mashirika ya msaada ya ndani na ya kimataifa yanayotaka kuwasaidia watu wa Somalia kufanya kazi katika maeneo yote kuwanusuru wale walioathirika. Pia aliyaomba mashirika ya msaada kutoa msaada wa haraka katika maeneo mapya yaliyokombolewa kama vile Kismayu, Marka na Wanlaweyn, na pia katika sehemu za Beledweyne zilizoathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni.

Kufukuzwa kwa mashirika ya msaada za Kiislamu kwawaua njaa wahanga wa ukame
Abdifatah Mohamed, mkurugenzi wa operesheni wa Badbaado, ambalo ni shirika la msaada na maendeleo nchini Somalia, alisema al-Shabaab wanaifanya hali ya kibinaadamu nchini Somalia kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya amri yake ya kupiga marufuku mashirika ya msaada ya kimataifa.

"Al-Shabaab ndiyo inayobeba dhamana ya kuzorota kwa hali ya kibinaadamu nchini Somalia kwa sababu inazuia upitishaji wa msaada kwa maeneo yaliyoathirika," Mohamed aliiambia Sabahi.

Mohamed alisema kwa al-Shabaab kuyafukuza mashirika ya msaada inakusuda kuwafanya watu wafe njaa, hasa wahanga wa ukame. "Hapo zamani, al-Shabaab iliyapiga marufuku mashirika ya msaada yasiyo ya Kiislamu kufanya kazi kwa sababu ilidai mashirika hayo yangelifanya shughuli za kutia mashaka zaidi ya zile za kibinaadamu. Ujanja huo, hata hivyo, haufanyi tena kazi baada ya kundi hilo kuifukuza Islamic Relief," alisema.

"Imekuwa wazi kwamba al-Shabaab haina huruma yoyote kwa wahanga wa ukame, kwani imezuia chakula na madawa kuwafikia na imeyafukuza mashirika ya msaada yaliyokuja Somalia kuwasaidia Wasomalia walio kwenye hali ngumu," alisema Mohamed.

"Pamoja na yote hayo, al-Shabaab inaweka vikwazo vya kikatili dhidi ya raia wanaoishi kwenye maeneo inayoyashikilia katika kiwango ambacho inawazuia wenye uhitaji mkubwa kwenda kwenye kambi za msaada katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali," alisema. "Huu ni ushahidi kwamba al-Shabaab haina ubinaadamu na haina hisia za kiutu inapowashughulikia wahanga wa ukame."

Maonyo ya uhaba wa chakula wa mara kwa mara
Ahmed Sheikh Muse, anayefanya kazi na Sardo ambalo ni shirika la ndani la msaada, alisema hali ya kibinaadamu nchini Somalia itazorota baada ya kufukuzwa kwa mashirika ya msaada ya kimataifa.

"Mavuno ya msimu uliopita yalikuwa madogo, hali iliyosababisha kupanda kwa bei za nafaka na chakula. Hili linawalazimisha watu wengi zaidi kutegemea chakula cha msaada, lakini amri ya al-Shabaab kupiga marufuku mashirika ya msaada katika maeneo inayoyadhibiti inafanya mambo kuwa mabaya zaidi," aliiambia Sabahi.

Kwa mujibu wa utafiti mpya wa shirika la kimataifa la Oxfam, upungufu wa chakula na maji katika baadhi ya sehemu za Somalia umefikia kiwango cha kutisha, pamoja na kupanda sana kwa idadi ya walio na utapiamlo, hasa katika mikoa ya Gedo, Bakool na Lower Jubba. Hata hivyo, Oxfam inasema kurudi tena kwa ukame ni jambo lisilotarajiwa.

"Kimbunga kikali cha msimu mbaya wa mvua uliopita, kushindwa kukua kwa mazao, kufa kwa wanyama na kukosekana kwa usalama kunamaanisha kwamba watu waliokuwa wameanza kujishika mwaka jana, sasa wanategemea msaada kwa kiasi kikubwa," alisema mkurugenzi wa Oxfam nchini Somalia, Senait Gebregziabher.

Oxfam ilifanya uchunguzi wa maoni ya watu kwa familia 1,800 katika maeneo 40 kwenye maeneo ya kati na kusini mwa Somalia mwezi wa Julai na Agosti ili kujua athari za ukame ulioikumba Somalia mwaka jana na kusababisha njaa iliyogharimu maisha ya maelfu ya watu. Oxfam iligundua kwamba asilimia 72 ya washiriki wa uchunguzi huo wa maoni wanahofia kwamba hakutakuwa na chakula cha kutosha kwa miezi minne ijayo, wakati asilimia 42 walisema walilazimika kuruka baadhi ya mlo

Post a Comment

Previous Post Next Post