BALOTELLI AIDAI MALIPO KAMPUNI YA UMBRO KWA KUTENGENEZA FULANA ZENYE MANENO YA "WHY ALWAYS ME"

Toto tundu Mario Balotelli ameambia kampuni ya vifaa vya michezo imlipe  baada ya kampuni hiyo kuuza Tshirt zenye msemo wake maarufu wa  "Why Always Me."

Mshambuliaji huyo wa Manchester City alivaa T-shirt yenye maneno hayo siku ambayo walicheza na mahasimu wao Manchester msimu uliopita.

Alivua jezi yake halisi kuwaonyesha mashabiki baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa 6-1 City dhidi ya United  - lakini Mario amekasirishwa baada ya kujua kwamba Umbro wanauza kopi ya T-shirt zake zenye maneno ya "Why Always Me".


Kutokana na hilo Balotelli akamwambia mtunza vifaa wa City Les Chapman aulizie malipo kutoka Umbro akiamini ana haki ya maneno yaliyotumika kwenye T-Shirts.


Leo alisema: "Mario alinifuata na kuniambia nini avae kwa ndani kabla ya mechi na United, nikamwambia hawezi kuvaa fulana yoyote itakayohusu kitendo cha kuchezea milipuko haswa katika dimba la United. Baada ya hapo dakika 10 mbele akaja kuniambia "Why Always Me"? Nikwambia safisana hiyo, na baada ya mechi tukaggundua kwamba Umbro walikuwa wanauza fulana kama zile zenye maneno yale yale.


"Mario akanituma niwapigie simu na kuulizia kuhusu malipo yetu lakini hakuna anayemiliki maneno." Pamoja na kutoswa kulipwa na Umbro, mshambuliaji huyo baadae alikaa chini na kutengeneza dili la kupromoti T-Shirts za mwanamuziki Tinchy Stryder na faida ya mauzo ya fulana hizo ilienda kwenye kusaidia jamii

Post a Comment

أحدث أقدم