Waziri
wa nchi za kigeni wa Marekani Hillary Clinton amesema kuwa yeye ndiye
aliyekuwa na jukumu la ulinzi katika ubalozi wa Marekani nchini Libya
ambapo balozi wake aliuawa mwezi uliopita.
Mauaji ya balozi huyo Christopher Stevens pamoja na wamarekani
wengine watatu limekuwa suala gumu sana katika siku hizi za mwisho za
kampeini za uchaguzi wa urais.
Kamati maalum ya Congress imearifiwa kuwa ombi la kutaka kuongezewa uslama katika ubalozi huo lilikataliwa na idara ya serikali.
Bi Clinton aliambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa kuhakikisha usalama wa ubalozi wa Marekani kote duniani ni wajibu wake na wala sio wajibu wa Ikulu ya White house.
Bi Clinton aliambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa kuhakikisha usalama wa ubalozi wa Marekani kote duniani ni wajibu wake na wala sio wajibu wa Ikulu ya White house.
Tulichohitajika kufanya katika idara ya mambo ya ndani ilikuwa kuangazia kilichokuwa kinatokea wala sio kuhusu nini kitatokea, Bi Clinton aliambia waandishi wa habari.
”Na hilo ndilo nilikuwa naangazia usiku na mchana kujaribu kuhakikisha kuwa tunajaribu kudhibiti hali kwa ushirikiano na idara zengine za serikali.” alisema Clinton
Serikali ya Rais Obama imekuwa ikikosolewa sana kuhusiana na shambulizi hilo dhidi ya ubalozi wa Benghazi hasa wakati huu ambapo kampeini za uchaguzi zinaposhika kasi.
BBC
إرسال تعليق