‘HEMEDI’ ATUPA KULE ISHU ZA KUFANYA MUZIKI, AELEKEZA NGUVU ZAIDI KWENYE FILAMU…!!

MSANII anayefanya filamu na muziki, Hemed Suleiman ‘Hemedi’, baada ya kuufanya muziki kwa miaka kadhaa na kutamba na ngoma kadhaa ikiwemo ‘Alcohol’, sasa ameamua kuuweka pembeni muziki na anazipeleka nguvu zake kwenye filamu kwani tasnia hiyo ndiyo iliyomtangaza zaidi.

Mwandishi wa DarTalk aliamua kumtafuta msanii huyo ili aweze kufunguka zaidi kuhusiana na ishu hiyo na baada ya kupatikana alidai kuwa ameamua kujiweka pembeni kidogo ili nguvu zake ziende zaidi kwenye filamu.

“Nimekaa pembeni nilichofanya mashabiki wangu wanajua, sitaki kuongea sana, hivi sasa napeleka nguvu zangu kwenye tasnia ya filamu zaidi kwani huku sina mpinzani anayeweza kunifunika,” alidai.

Alipoulizwa swali kuwa ameamua kukaa pembeni kwa sababu hana nyimbo za kuimba au wale aliyokuwa anaiba kazi zao wameisha, alijibu kuwa hayo maneno ya watu kwani mara zote huwa anafanya kazi kwa akili yake na wala hajawahi kujihusisha na kazi za wasanii wengine

Post a Comment

أحدث أقدم