KAZI KWELI:- SHUHUDIA PICHA ZA BAADA YA VURUGU MAENEO YA POSTA!


 Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo 
tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari
wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu. 



 Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianza


Picha zote na Happiness Mnale


Na Andrew Chale

WATU sita waliokuwa na nia ya  kuandamana kuelekea Ikulu wamekamatwa na Jeshi la Polisi.

kwa mujibu wa waandishi wa habari 
waliopiga kambi katika viunga vya Ikulu watu hao walifika mmoja mmoja 
kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na 
kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi 
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya 
Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.



Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha.

Post a Comment

أحدث أقدم