Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar, aliyemaliza muda wake,
J. Guninita, akiondoka ukumbini baada ya matokeo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mkuu wa CCM
Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa mchakato huo wa uchaguzi uliofanyika kwenye
Ukumbi wa PTA jana Oktoba 13, 2012.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo
na Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya
Mwenyekiti huyo kutangazwa rasmi kushika nafasi hiyo kwa kumshinda mpinzani
wake, J. Guninita kwa kura 310 kwa 214, katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba
13, kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa CCM
Mkoa wa Dar es Salaa, Hadija Faraji, wakati wa uchaguzi huo uliofanyika jana
Oktoba 13, 2012 kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,
waliohudhuria uchaguzi huo, akizungumza kusalimia wanachama kabla ya kuanza kwa
mchakato huo.
Wagombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam, kutoka (kushoto) ni Ramadhan Madabida, Chizii na Guninita, kabla ya
kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, akipiga
kura.
Ramadhan Madabida akipiga kura.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika
jana Oktoba 13, 2012 kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba na kutangazwa mshindi
katika kinyang’anyiri hicho kwa kupata jumla ya kura 310, huku mpinzani wake J.
Guninita akipata kura 214.
Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida, akizungumza baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika
jana Oktoba 13, 2012 kwenye ukumbi wa PTA, jijini.
Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida (kulia) akipongezwa na
aliyekuwa mgombea mwenzake katika kinyang’anyiro cha uchaguzi , huo, J.
Guninita, baada ya kutangazwa matokeo na kumsinda kwa jumla ya kura 310 kwa
214, katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa PTA jana Oktoba 13, 2012.
Baadhi ya mashabiki wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa
Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na wanachama wa CCM, wakishangilia na
kufurahia baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi.
Sehemu ya mashabiki na wanachama wa Madabida
wakishangilia ushindi wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar, Badabida.
Mashabiki na wanachama wa CCM, wakimsindikiza
mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar, Ramadhan Madabida baada ya kutangazwa
mshindi katika kinyang’anyiro hicho jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee wa CCM.
Baadhi ya wanaCCM mkoa wa Dar es Salaam wakimpongeza Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
إرسال تعليق