MSIBA MWINGINE TENA IRINGA ,MMOJA WA WASAMARIA WEMA ALIYEKUWA AKIMUUNGUZA MTOTO JULIANA AFIWA NA MUME WAKE MWANAHABARI WA NURU FM

Mmoja kati ya  wasamaria wema ambaye  alimsaidia mtoto Juliana Mwinuka kufikishwa katika matibabu Jemida Kulanga ambaye ni mke wa mwanahabari Mlongwa Mkuchu amepatwa na msiba mkubwa kwa kufiwa na ubavu wake Mlongwa ( hapa alikuwa katika Hospitali ya CCBRT baada ya  kumfikisha Hospitali mtoto Juliana huku akiwa na mgonjwa wake pia) 


Jemida  Kulanga (kulia) akiwa na wasamaria wengine na mtoto Juliana Mwinuka  siku alipofikishwa katika matibabu

Hili ndilo shirika ambalo  pia ni wamiliki wa radio Nuru Fm ambalo mwanahabari marehemu Mlongwa Mkuchu alikuwa akifanyia kazi (tunaomba radhi kwa  kukosa picha yake katika maktaba ya mtandao huu)

Taarifa  nyingine  kutoka mkoani Iringa ambazo  zimethibitishwa na meneja  wa  kituo cha radio Nuru Fm Victor Chakudika kwa mtandao  huu  wa
www.francisgodwin.blogspot.com zinadai  kuwa aliyepata kuwa mwandishi wa shirika la IDYDC katika ukusanyaji wa habari za vijana ,shirika ambalo linamiliki kituo hicho cha Radio Nuru Fm Mlongwa Mkuchu amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Ocen Road jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akitibiwa .

Chakudika amesema  kuwa Mlongwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kansa katika mgongo wake na kupelekwa katika Hospitali hiyo.


Mbali ya mchango wa Mlongwa  kuwa mkubwa katika jamii enzi za uhai  wake bado Mlongwa atakumbukwa kwa mambo mbali mbali ya kijamii ambayo amepata  kuyafanya enzi  za uhai wake katika kuielimisha jamii ya mkoa  wa Iringa juu ya janga la UKIMWI kupitia mradi wa WANAUME TUWAJIBIKE .


Kwa wadau  wa mtandao huo msiba wa Mlongwa  pia ni pigo kubwa  kutokana na mchango mkubwa ambao mke wake Jamida Kulangwa ambao aliutoa kwa mtoto Juliana Mwinuka wa kijiji cha Mavanga Ludewa ambaye aliungua kwa moto na kuendelea  kutabika nyumbani kwa zaidi ya miezi sita bila kusaidia hadi mwanamke  huyo Jemida alipofikisha taarifa zake katika mtandao huu na kuanza kusaidia kabla ya kwenda kijijini kumfuata mtoto  huyo kwa kushirikiana na msamaria mwema mmoja mkazi wa jiji la Dar es Salaam na mkazi wa Ludewa  walikubali kujitolea kuacha shughuli zao na kwenda kumchukua mtoto huyo .


Hadi leo Jemeda anapatwa na tatizo  hilo ndie alikuwa msaada mkubwa wa  kumuuguza mtoto huyo akishirikiana na mdau  huyo mkazi wa jiji la Dar es Salaam na Jemida  alikuwa akimuuguza mtoto Juliana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliko sasa  huku akiendelea  pia kumuuguza mume  wake katika Hospitali ya Ocen Road hadi kifo kinapomkuta.


Mtandao  huu unaendelea kumpa moyo mdau Jemida Kulangwa  kupiga moyo konde katika kipindi hiki kizito kwake na kuwaomba  wadau  kuendelea  kumsaidia mtoto Juliana Mwinuka pia.

Post a Comment

أحدث أقدم