Mwandishi wetu alifanya mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya muziki wake pamoja na maisha kwa ujumla ndipo alipoitoa ishu hiyo, kwa madai kuwa wenaume wengi Bara wanapenda kutoka na mwanamke mrembo mwenye kila aina ya mvuto na ndiyo maana wanakuwa na tabia ya kuacha acha hovyo.
Alidai kuwa Zanzibar wanawake wengi ni wale ambao wanaovaa baibui muda wote na hawana tabia ya kuonyesha miili yao na ndiyo maana unakuta hata wanaume hawana tamaa ya kutamani kila mwanamke wanayemuona mbele yao.
“Hakuna wahalibifu kama wanaume wa Dar yani ukicheka tu umekwisha, unajua hii ni tofauti sana na wanaume wa Visiwani na nahisi inatokana na wadada wenyewe kuvaa nguo za mitengo mno ambazo huacha sehemu kubwa za mwili zikiwa wazi hivyo humfanya mtoto wa kiume atumie kila njia kukupata,” alidai.
إرسال تعليق