Mkurugenzi
wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa shukurani kwa Wadhamini
wakuu waliofanikisha Serengeti Fiesta 2012 kufanyika na kumalizika kwa
amani kwa mikoa takribani 12 nchini Tanzania ilhali tamasha hilo
likiacha alama ya maendeleo na chembe za changamoto ya ukuzaji uchumi
kwa wananchi wa mikoa iliyo kuwa kwenye ratiba.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki Bora kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL) Steve Gannon
ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012
kupitia bia yake maridhawa kabisa ya Serengeti Premium Lager pichani
kati anaeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo ya
SBL,Ephraim Mafuru.Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye kiota
cha maraha cha Escape Two,Mbezi beach jijini Dar.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki bora kwa
wadhamini wa mafuta vyombo vya barabarani GAPCO walioshiriki vyema
Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwa Mkuu wa Masoko wa GAPCO, Ben Temu
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akitoa shukurani za dhati kwa wadau mbalimbali waliofanikisha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwa namna moja ama nyingine.
Msanii
mkongwe wa muziki wa kizaz kipya a.k.a Bongofleva Sir Juma Nature
akimwimbia mmoja wa watangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha
Jahazi,Wasiwasi Mwabulambo. Katika hafla hiyo iliyokuwa ya aina yake
iliwajumuisha watu mbalimbali wakiwemo wasanii mbalimbali walioshiriki
tamasha la Serengeti fiesta 2012 na wadau wengine.(Picha na Gsengo wa http://gsengo.blogspot.com/)
إرسال تعليق