Tanzania inatarajia kuchukua hatua kama iliyochukuliwa nchini Kenya
ya kuzichinjia baharini simu zote za bandia ambazo nyingi ni za kichina
kwa kuzizima kabisa.
Taarifa hiyo imetolewa na kaimu meneja mawasiliano wa mamlaka ya
mawasiliano (TCRA) Semu Mwakyanjala ambaye amesema mamlaka hiyo itaanza
kwa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na umuhimu wa kununua simu halali.
Ameliambia gazeti la Daily News Jumapili kuwa hatua hiyo itachukuliwa
na nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Rwanda,
Uganda na Burundi.
Kuna taarifa kuwa makampuni mengi ya simu nchini Tanzania yameupokea
mpango huo kwa shingo upande kwa hofu kuwa yatapoteza wateja wengi.
Kwa upande wa tume ya mawasiliano ya Uganda (UCC) hatua hiyo ya kuzima simu bandia itafanyika mwishoni mwa mwezi November.
Post a Comment