Jemida Kulanga (kulia) akiwa na wasamaria wengine na mtoto Juliana Mwinuka siku alipofikishwa katika matibabu
Hili ndilo
shirika ambalo pia ni wamiliki wa radio Nuru Fm ambalo mwanahabari
marehemu Mlongwa Mkuchu alikuwa akifanyia kazi (tunaomba radhi kwa
kukosa picha yake katika maktaba ya mtandao huu) Taarifa nyingine kutoka mkoani Iringa ambazo zimethibitishwa na meneja wa kituo cha radio Nuru Fm Victor Chakudika kwa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com zinadai kuwa aliyepata kuwa mwandishi wa shirika la IDYDC katika ukusanyaji wa habari za vijana ,shirika ambalo linamiliki kituo hicho cha Radio Nuru Fm Mlongwa Mkuchu amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Ocen Road jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akitibiwa . Chakudika amesema kuwa Mlongwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kansa katika mgongo wake na kupelekwa katika Hospitali hiyo. Mbali ya mchango wa Mlongwa kuwa mkubwa katika jamii enzi za uhai wake bado Mlongwa atakumbukwa kwa mambo mbali mbali ya kijamii ambayo amepata kuyafanya enzi za uhai wake katika kuielimisha jamii ya mkoa wa Iringa juu ya janga la UKIMWI kupitia mradi wa WANAUME TUWAJIBIKE . Kwa wadau wa mtandao huo msiba wa Mlongwa pia ni pigo kubwa kutokana na mchango mkubwa ambao mke wake Jamida Kulangwa ambao aliutoa kwa mtoto Juliana Mwinuka wa kijiji cha Mavanga Ludewa ambaye aliungua kwa moto na kuendelea kutabika nyumbani kwa zaidi ya miezi sita bila kusaidia hadi mwanamke huyo Jemida alipofikisha taarifa zake katika mtandao huu na kuanza kusaidia kabla ya kwenda kijijini kumfuata mtoto huyo kwa kushirikiana na msamaria mwema mmoja mkazi wa jiji la Dar es Salaam na mkazi wa Ludewa walikubali kujitolea kuacha shughuli zao na kwenda kumchukua mtoto huyo . Hadi leo Jemeda anapatwa na tatizo hilo ndie alikuwa msaada mkubwa wa kumuuguza mtoto huyo akishirikiana na mdau huyo mkazi wa jiji la Dar es Salaam na Jemida alikuwa akimuuguza mtoto Juliana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliko sasa huku akiendelea pia kumuuguza mume wake katika Hospitali ya Ocen Road hadi kifo kinapomkuta. Mtandao huu unaendelea kumpa moyo mdau Jemida Kulangwa kupiga moyo konde katika kipindi hiki kizito kwake na kuwaomba wadau kuendelea kumsaidia mtoto Juliana Mwinuka pia. |
Post a Comment