|
Toleo la Kati na Tabitha |
|
Toleo la Mwisho amekumbatia Tabitha |
|
Wakiwa na 'mke wao' Tabitha |
|
Utapenda swaga zao |
|
Kipa wa Coastal Union, Jackson Chove akimpima uzito Tabitha |
|
Chove na Tabitha |
|
Juu ni Mze Jangala na Lulu na chini huku ni makachaa watatu |
WASANII wa kundi la Vituko Show la Tanga, Kazi Suleiman ‘Toleo
la Kati’ na Ally Bofu ‘Toleo la Mwisho’, kwa kushirikiana na Chamoyo, wametoa
wimbo uitwao Mamido, ambao muda si mrefu
utaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya Radio nchini.
Toleo la Kati, alisema jana kwamba, wimbo huo
wamerekodi katika studio za Gizzle Records mjini Tanga na wako mbioni kuufanyia
video, wakiwashirikisha wasanii wenzao wa Vituko Show, kama Lulu Matawalo ‘Baby
Brown’ na Tabitha Jacob ‘Mama Shotii’.
“Hii ngoma brother imesimama sana, we utaisikia ikitoka, tumepiga
mtindo wa R&B, yaani tumeharibu vibaya,”alisema Toleo la Mwisho.
Kwa nini wanajiita Toleo la Kati na la Mwisho; “Unajua Mungu
katika kuumba walemavu, mimi ni toleo la mwisho kabisa la walemavu, na
mwenzangu (Kazi), yeye ni toleo la kati,”alisema Ally Bofu.
Kundi la Vituko Show linaloongozwa na magwiji wa sanaa ya
uigizaji nchini, kama Mzee Jangala na King Majuto, limejizolea sifa za kutosha
ndani ya muda mfupi, kutokana na kuibua wasanii wakali kama Kitale na Sharo
Milionea.
إرسال تعليق