WAFUNGWA 120 WATOROKA JELA NCHINI LIBYA BAADA YA ASKARI KUPOKEA RUSHWA.

Wafungwa 120 wametoroka jela katika mji mkuu wa Libya – Tripoli, baada ya walinzi wa gereza kupokea hongo na kuwafungulia milango.
Msemaji wa kamati ya usalama nchini Libya amekaririwa akisema Abdel-Moneim al-Hurr amesema ni wafungwa wawili tu kati ya wafungwa hao ndio waliokamatwa tena.
 Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa idadi kubwa ya wafungwa kutoroka jela mjini Tripoli.
Wafungwa nchini Libya wanalalamika kwamba tangu vuguvugu lililomuondoa madarakani Rais Muamar Gaddafi,  mahakama zimeacha kushughulikia kesi zao

Post a Comment

Previous Post Next Post