Wafungwa
120 wametoroka jela katika mji mkuu wa Libya – Tripoli, baada ya
walinzi wa gereza kupokea hongo na kuwafungulia milango.
Msemaji
wa kamati ya usalama nchini Libya amekaririwa akisema Abdel-Moneim
al-Hurr amesema ni wafungwa wawili tu kati ya wafungwa hao ndio
waliokamatwa tena.
Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa idadi kubwa ya wafungwa kutoroka jela mjini Tripoli.
Wafungwa nchini Libya wanalalamika kwamba tangu vuguvugu lililomuondoa madarakani Rais Muamar Gaddafi, mahakama zimeacha kushughulikia kesi zao
إرسال تعليق