WAISLAM NCHINI WATOA TAMKO NA KULAANI VITENDO VYA UCHOKOZI WA KIDINI.

Sheikh kutoka Jumuiya na Taasisi za kiislamu Tanzania Ponda Issa Ponda (katikati) akitoa tamko mbele ya vyombo vya habari kuhusiana na kile walichokiita kadhia iliyotokea tarehe 10.10.2012 ya kunajisiwa kwa kitabu kitufu cha Qur’ani. Kushoto ni Imamu Mkuu wa Masjid Al-Amin Sheikh Ibrahimu Ghulaam na kulia ni Kiongozi wa Jumuia na taasisi na A-mallid Rajab Kitimba.

Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini Tanzania wametoa tamko kufuatia kitendo cha kijana Emmanuel Josefati (14) kukojelea kitabu kitukufu cha Qur’an na kusababisha mgongano wa mawazo miongoni mwa watanzania.
Katika tamko lao wamesema ‘Tunalaani Kitendo cha kukojolewa Qur’an Tukufu ambayo ni Kitabu Kitakatifu kwa Waislam Wote Duniani’.
‘Tunataka kusikia tamko la serikali la kulaani kitendo cha kukojolewa Qur’an’.
‘Tunataka serikali kukemea kitendo cha Jeshi la Polisi kushambulia Misikiti, waumini na Kuvuruga ibada’.
‘Tunalaani vitendo vya uchokozi wa kidini’.
‘Tunalaani matumizi ya matumizi ya nguvu kubwa dhidi ya raia yaliyofanywa na Polisi’.
‘Tumehuzunishwa sana na kitendo na kitendo cha kushambuliwa Misikiti na Makanisa kilichotokea Mbagala’.
‘Tunatoa siku 7 ndani ya siku hizi Waislamu wanaoshikiliwa na Polisi wapewe haki yao ya dhamana’.
Na. MO Blog

Post a Comment

أحدث أقدم