Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen.
Na. Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Abiria
wanne waliokuwa wakisafiri katika Daladala (Hiace) iliyokuwa inatokea
Dodoma kuelekea kijiji cha Mkanda wilayani Manyoni Mkoa Singida
wamepoteza Maisha katika tukio la ajali na kuwaacha abiria wengine kumi
na nane wakiwa majeruhi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kuwa ilitokea siku ya Jumapili tarehe 14/10/2012 majira ya saa kumi jioni (16:00hrs) katika Kijiji cha Uhelela Kata ya Bahi Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma katika barabara kuu ya Dodoma/Singida.
Bw. Zelothe Stephen alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T.518 AVQ aina ya SCANIA likiwa na tela lenye namba za usajili T.780 AVK lililokuwa linaendeshwa na Dereva TUTU ACKSON
mwenye umri wa miaka 23, Mkazi wa Chaduru, na gari namba T. 803 AHX
aina ya TOYOTA HIACE lililokuwa likiendeshwa na DANIEL JACKSON mwenye umri wa miaka 46, mkazi wa Dodoma.
Aliwataja
waliopoteza Maisha katika ajali hiyo kuwa ni abiria wanne waliokuwa
wakisafiri na Hiace hiyo ambao ni MASHAKA ELIA mwenye umri wa miaka (27)
ambaye ni kondakta,
mkazi wa Chang’ombe Mkoani Dodoma, MOSI MAUNDAA mwenye umri wa miaka
(55) mkazi wa wilaya ya manyoni, EZEKIELI MASALITO mwenye umri wa miaka
kati ya (40-45) mkazi wa Makanda wilaya ya Manyoni na DASTAN KIPINGU
mwenye umri wa miaka (35) ambaye hakufahamika ni mkazi wa wapi.
Mkuu
huyo wa Polisi Mkoa wa Dododma alisema Miili ya marehemu hao
imehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Bahi ikisubiri kuletwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa Uchunguzi zaidi wa Daktari,
wakati majeruhi wengine kumi na tano (15) wamelazwa katika Hospitali ya
Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.
“Katika ajali hiyo Abiria kumi na nane (18) walijeruhiwa akiwemo
Dereva wa Daladala hiyo, ambapo kati yao wanaume waliojeruhiwa ni 15
akiwemo mtoto mdogo mmoja na wanawake watatu (3).” Alifafanua Kamanda
Zelothe
Bw. Zelothe aliwataja waliotibiwa
na kuruhusiwa kuwa ni ESTER FUNGA mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa
Kintinku wilayani Manyoni, aliyejeruhiwa katika mkono wa kushoto na usoni, CHRISTINA DANIEL mwenye umri wa miaka (25) mhudumu wa hoteli, mkazi wa Ipagala, ambaye ameumia mkono wa kulia na mguu wa kulia na GREYSON OMARY mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni ambaye ameumia kichwani.
Aidha Kamanda Zelothe alitaja orodha ya majina ya waliojeruhiwa kuwa ni
DANIEL JACKSON @ NZOYA mwenye umri wa miaka (46) Dereva wa Toyota Hiace, mkazi wa Bahi road Dodoma, ANTONY CHAKA mwenye umri wa miaka (23) mkazi wa Makanda Manyoni, JOSEPH CHRISOPHER mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa Makanda, VENANCE MIRAJI mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, MASONGA BURUGE mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, PROTAS MWALUKO mwenye umri wa miaka (70) mkazi wa Makanda wilayani Manyoni na PEASON MAGUMILA mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Kibaigwa wilayani Kongwa.
Wengine ni TIMITA MADATILO mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Makanda wilayani Manyoni, MATONYA MWENDAUHEMBA mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa wilaya ya Bahi, MASHAKA ELIA mwenye umri wa miaka (27) mkazi wa Chang’ombe Dodoma, TITUS MTWEVE
mwenye umri wa miaka (32) mwalimu wa shule ya sekondari Manyoni, JUMA
SHABANI mwenye umri wa miaka (35) mkazi wa Makanda wilyani Manyoni,
SOPHIA LEMA mwenye umri wa miaka (52) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, RAMADHANI ABDALLAH mwenye umri wa miaka (38) mkazi wa wilyani Manyoni na mwanaume ambaye hajafahamika jina mwenye umri kati ya (35-40) ambaye hali yake ni mbaya.
Bw.
Zelothe Stephen alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha
ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori hilo ambaye aliigonga kwa nyuma
gari hilo la abiria iliyokuwa mbele yake na kuitoa nje ya barabara na kusababisha ajali hiyo, Dereva wa Lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam likielekea Kigoma amekamatwa na utaratibu wa kumfikisha mahakamani unaandaliwa.
Imetolewa na
POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
CONTACT:
Phone: 0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
Phone: 0712 360203, Silyvester Onesmo – Police Konstebo (PC)
Post a Comment