TOLEO LA KATI, LA MWISHO WA VITUKO SHOW WAREKODI WIMBO WA R&B

Toleo la Kati na Tabitha


Toleo la Mwisho amekumbatia Tabitha

Wakiwa na 'mke wao' Tabitha

Utapenda swaga zao

Kipa wa Coastal Union, Jackson Chove akimpima uzito Tabitha

Chove na Tabitha

Juu ni Mze Jangala na Lulu na chini huku ni makachaa watatu
WASANII wa kundi la Vituko Show la Tanga, Kazi Suleiman ‘Toleo la Kati’ na Ally Bofu ‘Toleo la Mwisho’, kwa kushirikiana na Chamoyo, wametoa wimbo uitwao Mamido, ambao muda si mrefu utaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya Radio nchini.
Toleo la Kati, alisema jana kwamba, wimbo huo wamerekodi katika studio za Gizzle Records mjini Tanga na wako mbioni kuufanyia video, wakiwashirikisha wasanii wenzao wa Vituko Show, kama Lulu Matawalo ‘Baby Brown’ na Tabitha Jacob ‘Mama Shotii’.
“Hii ngoma brother imesimama sana, we utaisikia ikitoka, tumepiga mtindo wa R&B, yaani tumeharibu vibaya,”alisema Toleo la Mwisho.
Kwa nini wanajiita Toleo la Kati na la Mwisho; “Unajua Mungu katika kuumba walemavu, mimi ni toleo la mwisho kabisa la walemavu, na mwenzangu (Kazi), yeye ni toleo la kati,”alisema Ally Bofu.   
Kundi la Vituko Show linaloongozwa na magwiji wa sanaa ya uigizaji nchini, kama Mzee Jangala na King Majuto, limejizolea sifa za kutosha ndani ya muda mfupi, kutokana na kuibua wasanii wakali kama Kitale na Sharo Milionea.

Post a Comment

Previous Post Next Post