Ruvu Shooting; Wenyeji mechi ya kesho |
MECHI
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga na Ruvu Shooting
uliopangwa kuchezwa kesho Uwanja wa Chamazi, sasa umehamishiwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alizungumza leo
kwamba, mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na maombi ya timu hizo
mbili kutaka mechi ichezwe Uwanja wa Taifa kutokana na sababu mbalimbali
ambazo zimeridhiwa na Kamati ya Ligi ya TFF, ikiwemo siku hiyo uwanja
huo kutokuwa na mechi.
Wambura
amesema katika mechi hiyo, itakayochezeshwa na refa Amon Paul kutoka
Mara ni viingilio vitakuwa Sh. 5,000 viti vya kijani na bluu, Sh. 8,000
viti vya rangi ya chungwa, Sh. 15,000 VIP B na C na sh. 20,000 kwa VIP
A.
Amesema
pia, Kamati ya Ligi imekataa ombi la timu ya Azam kutaka mechi zake za
nyumbani za ligi hiyo zichezwe dhidi ya Simba na Yanga zichezwe Uwanja
wa Chamazi kutokana na sababu za kiusalama.
Mechi
nyingine za kesho, Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, ambayo itachezeshwa na refa
Israel Nkongo atakayesaidiwa na Hamis Chang’walu na Omari Kambangwa,
wote kutoka Dar es Salaam.
Ligi
hiyo itaendelea tena Jumapili kwa mechi tatu, JKT Ruvu itaonyeshana
kazi na Azam FC kwenye Uwanja wa Chamazi, Mgambo Shooting itaikaribisha
Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Tanzania Prisons na
Toto Africans zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya.
إرسال تعليق