Kiungo
mshambuliaji wa Yanga, (kulia) akimtoka mchezaji wa
Azam Fc,
Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na
Niyonzima katika dakika ya 32 akiunganisha pasi nzuri kutoka kwa Jerry
Tegete, ambaye kwa leo ameonekana kupwaya zaidi na kukosa mabao kama
matatu ya wazi.
Kwa
ushindi huo Sasa Yanga inaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na jumla ya Pointi
39, wakifuatiwa na Azam wenye Pointi 36, nafasi ya tatu inashikiliwa na
Simba wakiwa na Pointi 31 nafasi ya nne ni Coast Union wenye Pointi 30,
huku Yanga wakiwa na mchezo mmoja kibindoni.
Baada
ya mchezo huo kumalizika wachezaji wa Azam, walimzonga mwamuzi wa
mchezo huo kwa kile walichodai kuonewa sakata lililookolewa na askari wa
usalam kwa kuwaondoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi mkali
huku wakipondwa na chupa za mikojo.
Post a Comment