NHIF yadondosha Bonge la hafla kuwashukuru Wanahabari kwa kufanikisha kongamano mkoani Mtwara.

12
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya kujipongezana na kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa Makonde mjini Mtwara,baada ya kumalizika kwa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika jana kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani humo.
2 
Maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka kulia ni Grace Michael na Dr. Ahena Mramba Rose Gabriel wakiwa katika hafla hiyo.
4 
Mkurugenzi wa Tathmini na Uhai wa Mfuko na Takwimu NHIF , Bw. Michael Mhando akifurahia jambo na Grace Michael Ofisa Masoko wa mfuko huo wakati wa hafla hiyo kulia ni ni Angela Mziray
5
Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Mgaya Kingoba wa Habari Leo na wenzake
7
Steven Mhina kulia akiwa na Angel Akilimali kushoto wote kutoka Radio Uhuru.
8
Wanahabari mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika hafla hiyo.
Ofisa wa Masoko wa NHIF Grace Michael wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari
11 
Kutoka kulia ni Catherin Sungura kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Grace Michael na Faraja Kihongole kutoka Chaenl Ten
14 
Hawa jamaa walikonga nyoyo za wanahabari kwa vichekesho vyao.
15
Gladness Mboma wa pili kutoka kulia na wanahabari wenzake wakiwa kaatika hafla hiyo.
17
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Moshi Chang’a akishukuru baada ya kupokea cheti chake kutokana na mchango wake wa NHIF katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba na kushoto ni Salome Manyama meneja wa tawi la NHIF makao makuu.
16
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Moshi Chang’a akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba na kushoto ni Salome Manyama meneja wa tawi la NHIF makao makuu
18 
Hapa ikiwa ni burudani kwa kwenda mbele
20 
Wanahabari wakacheza kwaito kama wanavyoonekana.
21 
Mchora Katuni King Kinya akitoa burudani jukwaani huku mpiga gitaa Yahya Mkango aliyewahi kufanya kazi na bendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post