Na Isaac Mwangi, EANA
Timu ya watu 40 yenye kujumuisha wajumbe kutoka nchi zote wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) isipokuwa Kenya wamepelekwa nchini humo kuwa
waangalizi katika uchaguzi mkuu ujao wa nchi hiyo utakaofanyika Machi 4, mwaka
huu.
Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi huo inaongozwa na Spika wa zamani wa
Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Abdulrahman Kinana wa Tanzania. Jukumu hilo
pia litaratibiwa na mbunge wa zamani wa EALA kutoka nchini Uganda, Lydiah
Wanyoto.
Akizunguma za waandishi wa habari jijini Nairobi juzi, Katibu Mkuu wa
EAC Dk Richard Sezibera alisema wajumbe wa timu hiyo wametoka katika maeneo mbalimbali
lakini wakiwa na lengo moja la kulikamilisha.
‘’Timu inajumuisha wajumbe toka EALA, Tume za Uchaguzi za Taifa,Tume za
Kitaifa za Haki za Binadamu na wawakilishi wa vijana toka Tasisi ya Mabalozi wa
Vijana wa EAC.Uteuzi pia uanzingatia uwiano wa jinsia na vijana.’’
Waangalizi hao Katibu Mkuu alisema,watakuwa waangalia jinsi kampeni
zinavyofanyika,uandikaji wa habari za uchaguzi na vyombo vya habari na sheria
zinazotawala utendaji wake, kazi ya uongozi wa uchaguzi wenyewe na wadau husika
katika kipengele hiki na utatuzi wa migogoro itakayotokea katika uchaguzi huo.
‘’Timu hiyo itakutana na kushauirina na wawakilishi wa wadau katika
uchaguzi huo na vyama vya siasa pamoja na wagombea wao na pia wawakilishi wa
vyama vya kiraia, waandishi habari na jumuiya za kimataifa,’’ alisema Dk.
Sezibera.
Timu ya EAC kwa mujibu wa Dk Sezibera, itaungana pamoja na timu ya Soko
la Pamoja toka Kusini mwa Afrika (Comesa) na Mamlaka ya Wadau wa Maendeleo
(IGAD) katika uratibu wa shughuli za uangalizi wa uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano huo Kinana alisema suala zima la uchaguzi huo
ni la Wakenya na jukumu la timu yake ni kuangalia yatakayotokea na kuandika
ripoti juu ya uchaguzi huo.
إرسال تعليق