Ikulu:- Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiweka
 shada la maua kwenye jeneza
Mzee Amos Kaguta
na kutoa heshima zake za mwisho.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana(Feb 24,2013) aliungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.




 Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa cnhi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 



Akitoa salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu. 



Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuthamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake.



Rais kikwete akiwa na mwenyeji
wake Rais Yoweri Kaguta Museveni
wa Uganda wakiweka udongo
kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta
 wakati wa mazishi yake yaliyofanyika
katika kijiji cha Rwakitura.
Kulia ni Mama Janet Museveni
.....................................................
Picha na habari na Freddy Maro
Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao. 



 Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda. Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo

Post a Comment

Previous Post Next Post