Wapiganaji waasi wa M23 ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali ya DR Congo
Na Martha Saranga Amini
Nchi kumi na moja za Afrika zimealikwa kusaini mkataba na Umoja wa
Mataifa wa mwishoni mwa juma hili kwa lengo la kukomesha vita
vilivyodumu kwa zaidi ya miongo miwili huko mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky alisema ijumaa kuwa kiongozi
wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon atafanya jitihada kupata mkataba
uliosainiwa Addis Ababa jumapili.
Nesirky ameongeza kuwa kama mpango utafanikiwa utawezesha uvamizi maalum
wa jeshi la umoja wa mataifa UN huko mashariki mwa Congo ili kupambana
na makundi ya waasi na kusaidia utatuzi wa masuala ya kisiasa.
Msema wa umoja wa mataifa ameongeza kuwa viongozi wa DR Congo, Angola,
Burundi, afrika ya kati, jamuhuri ya Congo, Rwanda, afrika kusini,Sudan
kusini,Tanzania, Uganda na Zambia ni miongoni mwa mataifa yaliyoalikwa.
Maraisi kadhaa wanatarajiwa kuhudhuria.
Via kiswahili.rfi.fr
إرسال تعليق