Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akiagana na maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini
Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa
leo jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji
saini Mpango
wa
Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es
salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais
Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na
kuzikwa kijijini kwake
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati)
na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete
wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya Februari 24,
2013.Picha na IKULU
Post a Comment