Timu
ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya
Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo
jioni katika Uwanja wa Taifa.
Bao
la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika
dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba
moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.
Bao
hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezu
mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba,
walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza
falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.
Aidha
mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo
hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha
maji ya kuwasha, huku vingozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa
wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo.
Hata
hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi
nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha
pili.
Post a Comment