Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta |
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amewata wakuu
wa mikoa nchini kuondoa woga na kusimama kidete, ili kukomesha vurugu
zinazoendelea nchini yakiwemo mauaji yanayotokana na imani za kidini.
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alitoa kauli hiyo jana
wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama Cha Wanasheria wa
Tanganyika (TLS) katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
Alisema kama wakuu wa mikoa hawatatimiza wajibu wao, migogoro na
visingizio vya imani za kidini vitaendelea kukithiri siku hadi siku.
Waziri huyo alisema amekuwa akishangazwa na hatua ya viongozi wa mikoa
kushindwa kuzima maasi hayo mapema licha ya kuwa na vyombo muhimu
vinavyowapa taarifa za haraka.
“Wakati mwingine ni uoga wa viongozi wetu, ama kwa kutokujiamini maana
jambo linaaza kwao na wao wanakuwa na mamlaka zote lakini wanashindwa
kuchukua hatua mapema hadi Waziri Mkuu au Rais aingilie kati, hii ni
aibu kweli,” alisema Sitta.
Waziri huyo aliwataka viongozi wa mikoa kujenga ujasiri na kuwa wepesi wa kukabili matatizo yanapotokea katika maeneo yao ili yasilete madhara makubwa katika jamii. Kuhusu wanasheria, alisema licha ya Tanzania kuwa na chuo kikongwe cha kisheria, lakini bado ina upungufu mkubwa wa wanasheria ikilinganishwa na nchi kama Kenya ambayo wanasheria wake walianzia kusoma Tanzania.
Waziri huyo aliwataka viongozi wa mikoa kujenga ujasiri na kuwa wepesi wa kukabili matatizo yanapotokea katika maeneo yao ili yasilete madhara makubwa katika jamii. Kuhusu wanasheria, alisema licha ya Tanzania kuwa na chuo kikongwe cha kisheria, lakini bado ina upungufu mkubwa wa wanasheria ikilinganishwa na nchi kama Kenya ambayo wanasheria wake walianzia kusoma Tanzania.
Alisema kwa sasa watu waliosajiliwa kama wanasheria nchini Tanzania ni 3500 wakati nchi kama Kenya imesajili wanasheria 11,000.
“Chuo cha Lumumba ndicho Chuo kikongwe katika Afrika Mashariki chenye
kutoa taaluma ya sheria, lakini hadi sasa sisi tunawasheria wachache
ikilinganishwa na nchi za wenzetu na hasa Kenya,” alisema.
Hata hivyo alisema kuwa mkatati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sasa
ni kufungua soko la pamoja kwa wanasheria, ili waweze kufanya kazi
katika nchi zote ndani ya shirikisho.
Kwa upande mwingine alisema changamoto kubwa itakuwa ni katika masuala
la lugha kwani bado Kiingereza kinaonekana kuwa na nafasi kubwa lakini
pia nchi kama Burundi wanatumia lugha ya Kifaransa.
Kwa upande wake, Rais wa TLS Francis Stolla, alikiri kuwa gharama za
kisheria bado ziko juu ikilinganishwa na watu wanaohitaji kuhudumiwa.
Wakati Sitta akieleza hayo, Shirika la Under The Same Sun (UTSS)
limeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kukomesha mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Limesema matukio hayo ya kikatili yanahusishwa na imani za kishirikina kwani mpaka sasa watu 72 wenye ulemavu wa ngozi wameuawa.
Chanzo: Mwanachi
إرسال تعليق