Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon |
Na Flora Martin Mwano
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki-Moon amelaani mauaji ya askari
mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika cha kulinda
amani katika jimbo la Dahfur nchini Sudani.
Kwa mujibu wa taarifa toka ofisi ya UN mjini Dahfur, Ban ametaka mamlaka
nchini humo kuhakikisha wauaji wanakamatwa na wanafikishwa katika
vyombo vya sheria.
Askari huyo aliuawa na wengine wawili walijeruhiwa baada ya kundi la
watu kuvamia kituo chao kilichopo karibu na mji wa Muhagiriya.
Walinda amani zaidi ya 40 nchini Sudani wameuawa katika kipindi cha
miaka mitano na miito mbalimbali imekuwa ikizidi kutolewa kwa wahusika
wa mauaji hayo kuchukuliwa hatua za kisheria.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
إرسال تعليق