BEN PO AZUNGUMZIA KUHUSU IMANI YAKE NA KILI AWARDS NA KAFUNGUKA PIA KUHUSU WALIOJITOA.....SOMA NA MSIKILIZE HAPA

Wakati story kubwa ya burudani Nchini kwa sasa ikiwa ni Kilimanjaro Music Awards kwa mwaka 2013 ambapo kupitia bia ya Kilimanjaro wanapewa tuzo wasanii ambao wamefanya vizuri kuanzia january 2012 hadi december 2012 kila msanii amejipanga na anaamini kivyake kuhusu Tuzo hizo.

Kwa Mwaka jan a tulishuhudia baadhi ya Wasanii wakijitoa kwenye Kili music awards wakidai kuwa Tuzo hizo haziegemei upande wa haki bali zimekuwa na kutotenda haki akiwemo pia Mtu mzima dully sykes na wengi, nmeongea na Msanii ambaye kiukweli amefanya na bado anafanya vizuri kwa sasa kupitia Muziki huu wa Kizazi Kipya namzungumzia ben Po ambapo nilitaka kujua kutoka kwake jinsi gani amejipanga na anavyoamini kuwa atashinda Tuzo kwa upande wa Rnb pekee au amejipanga vip ambapo yeye amejibu kuwa anachotegemea ni mafans wake kwani wao haswa ndio wanaojua ni kiasi gani amefanya kwa Mwaka Jana ila anaamini kuwa Kwa upande wake atafanaya poa.

Kwa upande wa Wasanii ambao walijitoa Pia ben Po nimemuuliza kuhusu imani yake na Kili awards ambapo kwa upande wake amesema wakati anaandika ngoma na kurecord hafanyi kwa ajili ya kili ila anafanya kwa fans wake kwa hiyo kwa watu kuandaa tuzo ni jambo zuri na kwamba haoni haja ya msanii yeyote kujitoa badala yake Wasanii wafanye kazi nzuri na Watu watakubali na kuthibitisha kuwa yeye anaappriciate Tuzo hizo.

KAONGEA MENGI SANA MSANII HUYO ILA PATA KUSIKILIZA MAHOJIANO YEKE NA DJ HAAZU MOJA KWA MOJA HAPO CHINI:-

Post a Comment

Previous Post Next Post