HATIMAYE Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo
katika kata nne za udiwani kwenye Jimbo la Arusha Mjini kutokana na
waliokuwa wakishikilia nafasi hizo kuvuliwa uanachama na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Uchaguzi utafanyika Juni 16 katika kata 26 zilizoko katika halmashauri 21 tofauti nchini, zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kifo, kujiuzulu, kufukuzwa au kuhama chama kwa waliokuwa wakiziongoza.
Sambamba na hilo, pia NEC imetangaza uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Chambani-Pemba kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Salum Hemed Hamisi aliyefariki Machi 28, mwaka huu.
Hata hivyo, Kata ya Sombetini ambayo aliyekuwa diwani wake, Alphonce Mawazo (CCM) alihamia CHADEMA, haikuorodheshwa katika kata hizo zinazopaswa kufanya uchaguzi mdogo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugrnzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba, uteuzi wa wagombea katika uchaguzi wa ubunge utafanyika Mei 17 na kampeni zitaanza Mei 18 hadi Juni 15.
Kwa upande wa wagombea wa udiwani, uteuzi utafanyika Mei 14 na kampeni zitaanza Mei 15 hadi Juni 15.
Kata hizo na halmashauri zake kwenye mabano ni Stesheni (Nachingwea), Nyampu Lukano na Lugata (Sengerema), Genge Tingeni (Muheza), Ibugule (Bahi), Langiro (Mbinga) na Manchila (Serengeti).
Nyingine ni Iyela (Mbeya), Mbalamaziwa (Mufindi), Ruzewe Mashariki (Bukombe), Mianzini (Temeke), Dalai (Kondoa), Minepa (Ulanga), Makuyuni (Monduli) na Bashnet (Babati).
Mallaba aliongeza kuwa kata nyingine ni Kimandolu, Elerai, Kaloleni na Themi (Arusha), Iseke (Singida), Dongobesh (Mbulu), Ng’ang’ang’e (Kilolo), Ifakara (Kilombero), Msanze (Kilosa) na Mnima (Mtwara).
SOURCE TANZANIA DAIMA

إرسال تعليق