‘Sijaacha muziki ila muziki wa Tanzania unakatisha tamaa’ (Audio)

253333_169146819825499_3790828_n

Rapper wa Weusi, Bonta aka Maarifa amekanusha taarifa zilizotangazwa jana kuwa ameacha muziki ili kuendelea na kazi yake ya siku zote ya udaktari.
Akiongea leo kwenye Exclusive 255 ya Bongo5, Bonta amesema chanzo kilichotoa taarifa hiyo kilimnukuu tofauti na kwamba hawezi kuacha muziki mpaka atakapoondoka duniani lakini amekiri kuwa muziki wa Tanzania unakatisha tamaa.
“Muziki wa Tanzania unakatisha tamaa, una vipindi vingi sana vigumu yaani vipindi vya kucheka huwa ni vichache,” amefunguka Bonta.
“Kwa mfano mimi nimefanya positive movements nyingi lakini response imekuwa ndogo sana, yaani appreciation ni ndogo. Na appreciation ndogo sio kwa fans mtaani, kwa fans mtaani ni kubwa. Kwa wadau wanaoniunganisha na hao mafans 

Post a Comment

Previous Post Next Post