Wapendwa
marafiki, yawezekana wenginenhamjafuatilia mjadala Bungeni leo na hivyo
mnaweza kusikia kupitia vyombo vya habari na hivyo kupata edited
version of my comments. Nawafahamisha kuwa nimekataa bajeti kwa kuwa
Bajeti haijatatua wala kuonyesha mwelekeo wa kutatua matatizo ya
wananchi wangu ambayo ni NJAA ENDELEVU kutokana na ukame wa mara kwa
mara na UMASKINI unaozidi kuongezeka kutokana na BEI DUNI YA MAZAO YA
KILIMO NA MIFUGO NA TIJA NDOGO KATIKA KILIMO. Nilitegemea Bajeti iwe na
Skimu zaUMWAGILIAJI kama jibu la mvua haba na pia PRICE STABILIZATION
FUND kwa bei ya Pamba. Aidha nilitegemea kungekuwa na mkakati wa
kuanzisha viwanda vya nguo ili kuwa na soko la ndani kwa pamba yetu!
Sjinyanga, ambayo kila siku kuna njaa hakuna skimu ya umwagiliaji na
maeneo yenye mvua kama Kigoma, Rukwa, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya nk
yenye mvua ndiyo yamewekewa skimu za umwafiliaji. Hili haliwezekani.
NIMEKATAA.
Post a Comment