Mwili wa Abel
Thobias (14) mkazi wa kijiji cha Kumtana ukiwa eneo la tukio baada ya kupigwa na radi na kufariki papo hapo.
|
Mwili wa Abel
Thobias (14) mkazi wa kijiji cha Kumtana ukifanyiwa uchunguzi na Madaktari baada ya kupigwa na radi,ukionekana
kuungua vibaya.
|
Mwanafunzi
wa darasa la sita katika shule ya msingi Kumtana wilaya ya Ngara mkoani
Kagera amekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi na wengine
15 kujeruhiwa huku 96 wakipoteza fahamu kutokana na mshituko wa tukio hilo.
Akizungumza
mara baada ya kutokea tukio hilo Afisa elimu shule za msingi wilayani
Ngara Bw.Simon Mumbee amemtaja mwanafunzi aliyepoteza maisha
kuwa ni Abel Thobias (14) mkazi wa kijiji cha Kumtana wilayani humo.
Bw.Mumbee
alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 22 majira ya saa 7 mchana wakati
wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na ratiba ya masomo na
papo hapo kulitokea mvua iliyoambatana na radi na kupiga chumba cha
darasa na mwanafunzi huyo kufariki dunia kutokana na majeraha ya makubwa ya
kuungua katika mwili wake.
Alisema kuwa
wanafunzi 15 walipata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao huku 96 wakipatwa
na mshituko kati yao wavulana ni 30 na wasichana 66 na wote walikimbizwa katika hospitali ya Nyamiaga iliyoko wilayani
Ngara kwa matibabu zaidi.
Post a Comment