Mbunifu
wa mavazi wa kimataifa kutoka Tanzania, Sheria Ngowi amesema miongoni
mwa sababu kubwa zinazochangia kukwamisha watu kwenye usaili wa kazi ni
uvaaji.
Akiongea na Bongo5, Sheria Ngowi amesema uvaaji wa mtu huwasaidia watu wanaofanya usaili kumtambua mtu huyo ni wa aina gani.
“Wewe unaenda kuomba kazi ya udaktari umevaa jeans, tshirt na unavuta
sigara, hata yule anayekupa kazi anajua huyu sio daktari mzuri, au
unaenda umelewa, anajua kabisa huyu hata kwenye duty ya usiku hawezi
akakaa ofisini sababu ni mlevi,” amesema Ngowi.
“Uvaaji unasimama kwa niaba ya wewe, sehemu yeyote. Ndio maana mtu
akivaa vizuri hutajua ana hela au hana hela, amekula au hajala, ana
matatizo ama hana matatizo. Kwahiyo mtu anapoenda kuomba kazi sehemu
ujue hiyo kazi inamhitaji awe vipi, achana na maswali utakayoulizwa,
unaweza kwenda interview ukadhani utaulizwa maswali hamsini lakini kwa
uvaaji wako ukaulizwa mawili, kwasababu kila kitu anakijua, hana doubt
na wewe.”
Msikilize zaidi hapa.
Chanzo:- http://www.bongo5.com
Post a Comment