Quick Rocka kuonesha uwezo wake wa kuimba kwenye My Baby ft. Shaa na Ngwair (exclusive audio)

BIhmWQhCIAIFSYf
Rapper anayefahamika kwa mtindo wake wa kurap haraka, Quick Rocka anatarajia kuachia wimbo wake mpya wiki moja kuanzia sasa ambao amewashirikisha Shaa na Ngwair.
Wimbo huo uitwao My Baby umetayarishwa na producer Manecky wa AM Records na Quick aka Switcher ataonesha uwezo wake wa kuimba.
“Ni wimbo wa mapenzi, sijawahi kutoa wimbo wa mapenzi tangia nimeanza kutoka, iko tofauti, pia sijarap humo nimeimba, something different kabisa, sio yule Quick waliyemzoea anayechana haraka haraka au nini, humo ni Quick mpya kabisa, nimeimba na Ngwair ndio kachana ,” amesema Quick.
“Nilifikiria kufanya wimbo wa mapenzi lakini nikaona njia nzuri ya kuongea na mtoto wa kike ni kumtengenezea maneno mazuri yenye melody nzuri ndio maana nikaimba.”

Post a Comment

Previous Post Next Post