Rapper
anayefahamika kwa mtindo wake wa kurap haraka, Quick Rocka anatarajia
kuachia wimbo wake mpya wiki moja kuanzia sasa ambao amewashirikisha
Shaa na Ngwair.
Wimbo huo uitwao My Baby umetayarishwa na producer Manecky wa AM Records na Quick aka Switcher ataonesha uwezo wake wa kuimba.
“Ni wimbo wa mapenzi, sijawahi kutoa wimbo wa mapenzi tangia nimeanza
kutoka, iko tofauti, pia sijarap humo nimeimba, something different
kabisa, sio yule Quick waliyemzoea anayechana haraka haraka au nini,
humo ni Quick mpya kabisa, nimeimba na Ngwair ndio kachana ,” amesema
Quick.
“Nilifikiria kufanya wimbo wa mapenzi lakini nikaona njia nzuri ya
kuongea na mtoto wa kike ni kumtengenezea maneno mazuri yenye melody
nzuri ndio maana nikaimba.”
إرسال تعليق