Habari zilizotufikia toka IFM- Dar es salaam ni kwamba mwanafunzi mmoja ambaye bado hatujafanikiwa kulipata jina lake amefariki dunia kwa kulishwa sumu katika chakula alicholetewa na mpenzi wake ambaye ni mke wa mtu......
Taarifa zaidi zinadai kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mke wa mtu ambaye mbali na starehe za kimapenzi alikuwa pia anampekea chakula cha jioni
Baada ya mchezo huo kudumu kwa muda, mume wa mwanamke aliusoma mchezo mzima na kuandaa tego la kuwaangamiza wote....
Habari zinadai kwamba Siku ya jumatano jioni mwanaume huyo aliwahi kurudi nyumbani na kufanikiwa kukinasa chakula kilichokuwa kimeandaliwa tayari kwa kupelekwa kwa huyo mwanafunzi ambaye alikuwa anatembea na mke wake.....
Baada ya kukinasa, alijifanya kuzuga na kupotezea...Mkewe alipotoka alikichukua na kukitia sumu chakula hicho na kisha kukiweka kama kilivyokuwa kimeandaliwa....
Lengo lake lilikuwa ni kuwamaliza wote maana alijua ni lazima akifika watakaa na kula pamoja.....
Mwanamke alipopeleka chakula hakukaa kula na badala yake alimwambia yule mwanafunzi kuwa mume wake amewahi kurudi siku hiyo hivyo hatoweza kukaa wale pamoja....Mwanafunzi huyo akakipokea na kukila na ndipo mauti yakamkuta
Habari toka chuoni hapo zinadai kwamba mwanafunzi huyo alikuwa ameshadisco lakini alikuwa amepewa nafasi nyingine ya kurudia mwaka wa pili , hivyo aliendelea kukaa mtaani kama mwanafunzi....
Mwili wa marehemu bado uko Muhimbili kwa uchunguzi zaidi baada ya polisi kuuzuia kuzikwa....
Hizi ni habari mbaya sana kwa wanafunzi wa chuo hicho maana ni jumatatu tu mwanafunzi mwingine alifariki katika hali ya kutatanisha baada ya kifo cha mpenzi wake miezi michache iliyopita....
Habari za ndani zaidi zinadai kuwa toka mwaka huu uanze mpaka sasa chuo cha IFM kimepoteza wanafunzi 12 huku wawili wakiripotiwa kuwa na hali mbaya zaidi katika hospitali ya Muhimbili....
Post a Comment